16 Aprili 2012 - 19:30

Kikundi cha kwanza cha wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kimeanza kazi zake nchini Syria, Kikundi hicho chenye watu sita kina jukumu la kujaribu kuangalia utekelezaji wa kusimamisha vita, na kuwasiliana na serikali na wapinzani kuhusu kazi zao.

Kiongozi wa kikundi hicho Bw Ahmed Himmiche anasema,

"tutajipanga ili tuweze kujiandaa na kufanya kazi yetu haraka iwezekanavyo……..ndio tuko hapa, walinda amani wote wana matumaini"

Wachunguzi zaidi wanatarajiwa kwenda Syria katika siku zijazo, na baadaye wanatarajiwa kufikia 200. Hata hivyo mapambano nchini Syria bado yanaendelea. Serikali ya Syria imesema makundi ya watu wenye silaha yamewashambulia polisi na kusababisha vifo vya watu tisa, wapinzani nao wamesema majeshi ya serikali ya Syria yameushambulia mji wa Homs kwa siku ya tatu mfululizo.